Kwenye ukurasa wake wa twitter Rais Magufuli ameandika ujumbe maalum wa kulipongeza jeshi hilo, kwa kufanikiwa kujijengea heshima ndani na nje ya nchi, pamoja na kutimiza wajibu wake wa kulinda amani ya nchi.
"Nalipongeza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kutimiza miaka 53 tangu kuanzishwa kwake, kwa kipindi chote hiki Jeshi letu limeendelea kutimiza wajibu wake ikiwa ni pamoja na kulinda amani ya nchi yetu, kwa uzalendo, umahiri, ushupavu, uadilifu na nidhamu ya hali ya juu na hivyo kujijengea heshima ndani na nje ya nchi yetu. Najivunia kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa JWTZ", aliandika Rais Magufuli.
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lilianzishwa mwezi Septemba mwaka wa 1964, ambapo lilichukua nafasi ya jeshi la Tanganyika Rifles lililorithiwa na ukoloni wa Kiingereza.
Alichokiandika Rais Magufuli kwenye ukurasa wake wa twitter.