Ole Nangole alikata rufaa hiyo dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk Stephen Kiruswa ya kupinga hukumu iliyotolewa Juni 29, mwaka jana katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha na Jaji Sivangilwa Mwangesi aliyeamuru uchaguzi urudiwe kutokana na upungufu uliyojitokeza.
Naibu Msajili wa mahakama hiyo, Ester Mkwizu alisema mahakama hiyo imetupa rufaa hiyo kwa kuwa ina upungufu wa kisheria baada ya kukosekana kwa kielelezo namba nne na namba nane kwenye kumbukumbu ya rufaa.
Kwa mujibu wa Wakili wa Dk Kiruswa, Edmund Ngemela alidai mahakama imekubaliana na hoja za wajibu rufani kuwa ili mahakama ipitie ushahidi upya uliotolewa mbele ya Jaji Mwangesi, kwamba vielelezo vikikosekana ni lazima itupiliwe mbali.
Dk Kisurwa ambaye aliwakilishwa na mawakili Ngemela, Dk Masumbuko Lamwai na Daudi Haraka, alipinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Nangole katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, kwa hoja za kuwepo kwa wapiga kura kutoka nchi jirani ya Kenya walioletwa na Ole Nangole.
Pamoja na madai hayo ilidaiwa pia Chadema ilitumia magari kusindikiza na kubeba masanduku ya kupigia kura, Mkurugenzi wa Uchaguzi kutangaza matokeo baada ya mgombea wa CCM kutolewa nje na kutokea kwa vurugu ndani ya chumba cha kuhesabu matokeo.
Aidha kutokana na madai hayo, Jaji Mwangesi aliamuru kwamba kwa kuzingatia kanuni, sheria na ushahidi uliotolewa mahakama imetengua shauri hilo na kwa kujiridhisha kwamba mchakato mzima haukuwa wa haki na huru hivyo mahakama inaamuru uchaguzi urudiwe upya.
Tayari Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshatangaza kujiweka sawa kwa uchaguzi huo mdogo utakaofanyika baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza tarehe