Msigwa: "Msukuma povu la nini, waache polisi wafanye kazi, Kumbe pana umaa ee na bado"

Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Peter Msigwa amefunguka na kumtaka Mbunge na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Joseph Kasheku Musukuma kuacha kutoa povu na kutulia ili polisi wafanye kazi yao

Msigwa amesema hayo siku moja baada ya Mbunge Joseph Kasheku Musukuma kumlalamikia RPC wa mkoa wa Geita kuwa ana roho mbaya na hakutumia busara kumkata yeye Kama Mwenyekiti wa CCM mkoa Geita kwa kumfuata na kumshika kama mwizi na kulala rumande bali alipaswa kumfuata kimstaraabu wakaongea na kuona namna ya kulitatua tatizo hilo.
Kutokana na malalamiko ambayo ameyatoa Mbunge wa Geita, Peter Msigwa amemweleza kuwa anapaswa kutulia na kuwaacha polisi wafanye kazi yao huku akimweleza kuwa kumbe vitendo wanavyofanya polisi kukamata viongozi kinaumiza. 
"Msukuma povu la nini, waache polisi wafanye kazi, Kumbe pana umaa ee na bado" alisema Peter Msigwa 
Mbunge Joseph Msukuma kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) amekuwa ni Mbunge wa kwanza wa kukamatwa na jeshi la polisi na kulala rumande kwa masaa 24 lakini pia Mbunge huyo amewaka rekodi nyingine kuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa CCM wa kwanza kukamatwa na kulazwa ndani. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo