Mtatiro ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa facebook baada ya dakika chache kupita kutolewa uamuzi wa kesi ya uchaguzi wa rais nchini Kenya katika Mahakama ya Juu ilipofunguliwa kesi hiyo na kuanza kusikilizwa tokea Agosti 26, 2017 baada ya Muungano wa vyama vya upinzani (NASA) kuishtaki Tume ya Uchaguzi (IEBC) kwa kile walichokidai tume hiyo ilifanya udanganyifu juu na kumpa ushindi Uhuru Kenyatta.
"Kenya ni taifa tunalolidharau kwa sababu ya siasa la kikabila lakini Kenya ni taifa litakalo kuwa mwalimu wa siasa na demokrasia duniani. Hata Marekani sasa watajifunza kupitia Kenya",aliandika Mtatiro.
Taifa la Kenya limeingia katika historia mpya kwa nchi za Afrika kwa kuweza kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu wa rais baada ya Mahakama ya Juu kuamuru kurudiwa kwa uchaguzi huo ndani ya kipindi cha siku 60 tokea sasa baada ya Tume ya uchaguzi kudaiwa kukiuka Katiba na Sheria katika baadhi ya mambo na hivyo kuathiri matokeo ya uchaguzi.