AUDIO: Licha ya Katazo, Magunia ya Mkaa yakamatwa yakitoroshwa Makete

Lori hilo lilivyokamatwa katika Kijiji cha Kisinga Makete likiwa na magunia ya Mkaa




Agizo la halmashauri ya wilaya ya Makete Mkoani Njombe la kupiga marufuku kusafirisha mkaa Nje ya wilaya bado lipo pale pale na utekelezaji wa agizo hilo utaendelea kusimamiwa siku hadi siku

Hii inafuatia siku za hivi karibuni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mh. Egnatio Mtawa kukamata lori lenye magunia 170 ya mkaa likiwa kwenye harakati za kuusafirisha makaa huo kwenda jijini Dar Es Salaam

Tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Kisinga ambapo baada ya kulikamata lori hilo lenye namba za Usajili T 957 ATJ hali ya mabishano ilijitokeza

Hali hiyo ilimfanya mwenyekiti Mtawa kutoa maagizo kwa afisa mtendaji wa kijiji cha Kisinga kuwa lori hilo lisiondoke na alikute Makete wilayani kwenye ofisi za halmashauri

BLOG HII imemtafuta Afisa Misitu kutoka wakala wa Misitu TFS wilaya ya Makete Bw. Moses Ndiwu amesema kwa sasa kuna idadi ya watu tisa walioruhusiwa kusafirisha mkaa waliokuwa wameuhifadhi kwa muda maalum na wakimaliza hawatapewa tena kibali cha kusafirisha mkaa kama sheria ndogo ya halmashauri inavyosema

Kuhusu mkaa uliokamatwa kwenye lori uliokuwa tayari kusafirishwa kwenda jijini Dar Es Salaam Afisa huyo amelitolea ufafanuzi kwa kusema kuwa mkaa huo ulinunuliwa miongoni mwa mwanakikundi 9 waliopewa ruhusa ya kumalizia kusafirisha mkaa walionao

Sikiliza sauti hizo hapo chini kwa kubonyeza Play>>>>>>


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo