Na Karama Kenyunko,
Blogu ya jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu
Mkazi Kisutu, imesema October 4 mwaka huu, itatoa uamuzi kama Mbunge wa Singida
Mashariki Tundu Lisu(Pichani) anayekabiliwa na kesi ya uchochezi ana kesi ya kujibu au
la.
Hakimu Mkazi
Godfrey Mwambapa amesema hayo leo baada ya upande wa mashtaka uliokuwa
ukiongozwa na wakili wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi kufunga ushahidi wao kwa
kuita mashahidi watano.
Kabla ya hayo, Lisu
alidai kuwa, kwa ushahidi uliotolewa mahakamani hapo ameona kabisa kuwa hana
kesi ya kujibu. Hata hivyo, Hakimu Mwambapa amesema ni jukumu la Mahakama
kuamua kama mshtakiwa anakesi ya kujibu au la.
Aidha Mahakama
imezitaka pande zote mbili, ile ya mashtaka na ya utetezi Septemba 18,
kuwasilisha hoja zao kama mshtakiwa anakesi ya kujibu au la.
Katika kesi hiyo,
Lissu anakabiliwa na kesi ya uchochezi ambapo mapema mwaka huu, akiwa katika
viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alitoa kauli za uchochezi kuwa,
“Mamlaka ya Serikali mbovu ni ya kidikteta uchwara inahitaji kupingwa na kila
Mtanzania kwa nguvu zote, “huyu diktekta uchwara lazima apingwe kila sehemu”.
Kama uongozi utafanywa na utawala wa kijinga nchi inaingia ndani ya giza
nene.’’