VIDEO: Mtoto Ukiteketeza soko la Sido Mbeya

Taarifa zilizotufikia hivi punde kutoka kwa Ripota wetu jijini Mbeya,zinaeleza kuwa Soko la Sido lililopo mkabala na maeneo ya Mwanjelwa linateketea kwa moto hivi sasa,Taarifa zinaeleza kuwa chanzo cha moto huo bado hakijajulikana mpaka sasa.


Kwa mujibu wa Ripota wetu aliyepo eneo la tukio,anaeleza kuwa  Moto huo ulianza kuwaka mnamo majira ya saa tatu usiku huu na kusababisha tafrani kubwa kwa baadhi ya watu waliokuwepo maeneo hayo,ambao nao walionesha juhudi zao za kushriki kuuzima,lakini kwa bahati nzuri kikozi cha zima moto kikawa kimeishawasili na kuendelea kupambana na moto huo uliokuwa ukiwaka kwa kasi kubwa mpaka hivi sasa tunapoingia mitamboni.




Kama vile haitoshi katika kuongeza nguvu za kiusalama eneo hilo,Kikosi kutoka jeshi la Polisi la mjini Mbeya tayari nalo liliwasili katika eneo hilo katika suala zima la kuhakikisha ulinzi na usalama wa mali za watu unaimarika .

Angalia video hii:-


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo