MAWAKILI wa chama cha mawakili Tanganyika (TLS) mkoa wa Iringa wameugomea mgomo uliotangazwa na Rais wao Tundu Lisu kufanyika leo nchi nzima.
Mgomo huo ambao ulitarajiwa kuanza leo nchini umekwama kufanyika baada ya mawakili kufika mahakamani kuendelea na kesi kama kawaida huku wakidai njia zilizotumika kutangaza mgomo huo si sahihi ni za kidkteta hazijawashirikisha na hivyo hawapo tayari kuwagomea wateja wao.
Wakizungumza leo mtandao wa matukiodaimaBlog katika viwanja vya mahakama kuu kanda ya Iringa mara baada ya kumaliza shughuli zao za kutetea wateja wao katika kesi zao mahakamani hapo mawakili hao walisema kuwa wamefika kuendelea kuwatetea wateja wao kama kawaida na wataendelea kuwasikiliza wateja wao na sio mtu mmoja ama kikundi cha watu wachache ambao wanataka kukifanya chama chao cha TLS kuwa ni chama cha wanaharakati na sio chama cha mawakili tena . Angalia video hii hapa chini:-