Afikishwa mahakamani kwa kusambaza picha za utupu


Mkazi wa Tazara Magorofani,  Shaban Biro (47), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala , kujibu shtaka la  kusambaza  na kuonyesha picha za utupu katika mitandao ya kijamii.

Biro (47), alifikishwa mahakamani hapo leo  na kusomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Flora Mjaya.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Glory Mwenda, alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa Machi, 2016 mtaa wa Kilosa uliopo wilaya ya Ilala.

Inadaiwa mshitakiwa alisambaza picha hizo kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia simu ya mkononi aina ya Huawei  ambazo zilikuwa zinamwonyesha Nuru Awadhi akifanya mapenzi.

Mshitakiwa alikana shtaka na hakimu Mjaya alihirisha kesi hiyo hadi April 17,2017 itakapotajwa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo