Mwanafunzi wa kidato cha pili, ‘jina linahifadhiwa’ (15) mkazi wa Mbagala, jijini Dar es Salaam amekatishwa masomo yake baada ya kupewa ujauzito.
Mwanafunzi huyo mwenye ujauzito wa miezi mitano amepiga stori na #Cloudsfmtz na kusema kuwa kijana aliyempa ujauzito huo mwenye umri wa miaka 19 ametoweka na hajulikani alipo baada ya kugundua msichana huyo ana ujauzito.
‘Nilikutana na kijana huyo wakati nilipokuwa nakwenda kuchota maji alikuwa akiniambia anataka kuonana na mimi, nikamwambia sina muda lakini akanieleza atanisubiri baada ya kutoka shule, kesho yake tukaonana akaniambia atanipa chochote ninachotaka atanipa, tulikuwa tukikutana nyumbani kwa shangazi yake’’ Alisema mwanafunzi huyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni,Hashim Mgandilwa ameingilia kati kati suala hilo na kusema atahakikisha kijana huyo atakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria