Dkt. Vincent Anney amewataka watu wa makanisa kuwasilisha kwake ratiba yao ya ibada kwa kuwa wana haki ya kuabudu na amewataka pia wanaotaka kufanya mikutano ya injili lazima wapate kibali kwa ajili ya mikutano hiyo.
"Wana haki ya kuabudu wawasilishe ratiba ya zao za kuabudu katika ofisi yangu ya Mkuu wa Wilaya wakitaka kufanya mikutano ya nje wapate kibali, mimi nimepiga marufuku muziki wa holela uwe wa dini wa kawaida, muziki wa dansi ambao watu wanapiga masaa 24 kuna haki za raia wengine vinavunjwa na hao wenye makanisa ambao wanahubiri masaa 24" alisema Mkuu wa Wilaya ya Musoma