Kamanda Mambosasa amesema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na kudai polisi yoyote ambaye anasema amekuja kumkamata mtu kwa 'order' kutoka juu ni wazi kuwa polisi huyo ni mbabaishaji na hajui anachotenda.
“Katika kipindi changu hutasikia kauli ya 'order' kutoka juu na ukisikia ikatie rufaa, nipigie niambie kuna mtu anataka kuchezea uhuru wangu, Ukisikia askari anasema 'order' kutoka juu ujue huyo hajiamini na pengine ni mbabaishaji hajui anachotenda" alisema Mambosasa
Aidha Kamanda Mambosasa amedai kuwa jeshi la polisi linafanyakazi kwa kuzingatia katiba, sheria na kanuni pamoja na miongozo inayoliongoza jeshi la polisi na si kitu kingine.