Askari polisi wa kitengo cha intelijensia katika mkoa wa Kagera aliyefahamika kwa jina la Mussa Salum Musanya amekutwa amefariki baada ya mwili wake kuokotwa ukielea kwenye ufukwe wa ziwa Victoria katika eneo la Kiroyera manispaa ya Bukoba.
Askari huyo wa polisi ambaye ameopelewa kwenye maji huku mwili wake ukiwa na sare za jeshi la polisi alitoweka nyumbani kwake na kupotea katika mazingira ya kutatanisha siku tatu zilizopita na kila walipomtafuta hakuweza kupatikana mpaka mwili wake ulipokutwa ukielea kwenye fukwe ya ziwa Victoria.
Jeshi la polisi linaendelea kufanya upelelezi wa tukio hilo.