Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemuachia huru Mkuu wa Kitengo cha Habari wa klabu ya Simba Haji Manara kuendelea na majukumu yake kama kawaida.
Hayo yameweka wazi na Mwenyekiti wa Kamati ya nidhamu Abasi Tarimba katika mkutano wake na waandishi wa habari mchana wa leo.
Manara alifungiwa na Shirikisho hilo baada ya kubainika utovu wa nidhamu wa kutoa matamshi yasiyo na staha kwa viongozi wa TFF pamoja na vyombo vya uongozi wa mchezo huo ambapo alihukumiwa muda wa miezi 12 na kutakiwa kulipa faini ya shilingi milioni tisa adhabu iliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya TFF Wakili msomi Jerome.