Kwaniaba ya Waislamu Mwenyekiti wa taasisi ya Imam Bukhari, Sheikh khalifa Khamisi ameeleza kwa masikitiko makubwa Madhira ambayo wameendelea kufanyiwa watuhumiwa wa kesi mbalimbali za ugaidi hapa nchini hususani Masheikh wa Uamsho waliokamatwa Visiwani Zanzibar mwaka 2012, ambapo amemuomba Rais Magufuli kuingilia kati ili watuhumiwa hao wapewe haki yao kwani wamekaa mahabusu muda mrefu.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, Sheikh Khalifa amesema Watuhumiwa hao wanafanyiwa manyanyaso wakati mahakama bado haijawahukumu na kuwakuta na makosa wanayotuhumiwa, jambo ambalo limewafanya kutoa tamko hili...