July 16, 2017 Rais Magufuli amesali Ibada ya Jumapili ya 15 ya mwaka wa Kanisa iliyofanyika katika Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato Mkoani Geita na ameendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo.
Katika harambee hiyo Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli amefanikiwa kuchangisha fedha taslimu kiasi cha Shilingi Milioni 13, ahadi Shilingi 920,000/=, mifuko ya saruji 33 na malori 2 ya mchanga.