Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) anayemuunga mkono Prof. Ibrahim Lipumba ameeleza kusikitishwa na matamko mbalimbali yanayotolewa na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kuingilia kati mgogoro wao kwa kile alichokisema ni nia ya kukichafua chama chao kwa upande wa Tanzania Bara .
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo Julai 12, Sakaya amekilaumu chama CHADEMA na viongozi wake kushirikiana na Katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Hamad.
Aidha Sakaya amesema mipango hiyo ni pamoja na kuvamia ofisi ambapo sasa wameenda mbali zaidi na kuamua kujitokeza kwenye kesi zilizofunguliwa na washirika wao dhidi ya viongozi wa CUF.
Hata hivyo amekiomba chama cha CHADEMA kujikita katika kutafuta sababu za wanachama na viongozi wao kuhama katika chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na si kuingilia kati mgogoro wao ambao kimsingi hauwahusu.
Amesema kuwa uwepo wa viongozi wa chadema mahakamani katika kesi zilizofunguliwa ni ushahidi tosha wa vikao vyao vya maazimio kuwa wanahusika na mgogoro unaohusu chama chao.