Mwanamke aliyejeruhiwa Kibiti apatiwa matibabu

Mwanamke aliyejeruhiwa kwa risasi usiku wa kuamkia juzi katika kijiji cha Ruaruke, wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani, Tabia Mbonde anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Mchukwi, kinyume na taarifa zilizoenea kwamba amefariki.

Awali iliarifiwa kuwa watu wasiojulikana walimuua kwa kumpiga risasi, mkazi wa Kijiji cha Ruaruke, wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani, Ramadhani Mzurui, usiku wa kuamkia juzi na kumjeruhi mguuni kwa risasi mke wa marehemu ambaye alikimbizwa hospitali kwa matibabu.

BLOG HII ilifunga safari mpaka hospitalini hapo na imefanikiwa kumpata majeruhi huyo ambaye  alishuhudia mumewe akiuawa kwa risasi na yeye kukimbilia msituni baada ya kupigwa risasi tano mguuni.

Baada ya tukio hilo, mama huyo anadai alianguka msituni ambako alikuja kuchukuliwa na Wasamaria wema na kupelekwa hospitali.

CHANZO; GPL


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo