Mkurugenzi wa 93.7 Efm Dar Es Salaam, Francis Ciz, akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Seth Katende ‘Bikira wa Kisukuma’ ambaye alikuwa Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha 93.7 EFM kupitia kipindi cha Ubaoni, wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika katika Makaburi ya Kinondoni jioni ya leo jijini Dar.
Mzee Katende (katikati) akiweka shada la maua katika kaburi la mtoto wake Seth Katende maarufu kama Bikira wa Kisukuma.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Bi.Zawadi Msalla akienda kuweka shada la maua katika kaburi la Marehemu.
Baadhi ya Ndugu jamaa na Marafiki wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kushiriki Mazishi ya Marehemu Seth Katende.
MWILI wa marehemu Seth Katende ‘Bikira wa Kisukuma’, aliyekuwa mtangazaji wa kituo cha redio cha Efm, kipindi cha Ubaoni, umeagwa katika viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam, ambapo baada ya kumalizika kwa shughuli hizo, safari ya kuelekea kwenye makazi yake ya milele, kwenye Makaburi ya Kinondoni ilianza ambapo hatimaye maziko yamefanyika mchana wa Julai 12, 2017.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi