Chanzo cha kuaminika ndani ya Simba kimethibitisha Mbonde kujiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili.
“Kweli Mbonde amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar na atakuwepo kwenye kikosi chetu cha msimu ujao.”
www.shaffihdauda.co.tz imemtafuta kocha mkuu wa Mtibwa Sugar Zubery Katwila ili kujua kama anataarifa yoyote kuhusu mchezaji wake kusaini mkataba na Simba kwa ajili ya msimu ujao.
“Mimi sina taarifa rasmi, sijapewa taarifa yoyote kuhusu hilo. Hata mimi nimeona kwenye mitandao na kupigiwa simu na waandishi wakiniuliza kuhusu suala hili,” – Zubery Katwila.
“Hadi sasa bado sina taarifa kutoka kwa klabu kwa hiyo siwezi kukwambia chochote.”
Mbonde alikuwepo kwenye kikosi cha Stars ambacho kimeshiriki michuano ya COSAFA 2017 ambacho kimemaliza katika nafasi ya tatu kwenye michuano hiyo huku Mbonde akiwa ni miongoni mwa wachezaji waliocheza mechi zote (6) kuanzia hatua ya makundi.