Hayo yamebainishwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Madadi ambapo amesema Bocco ameondoka jana nchini kuwafuata wenzake walioko huko kwa lengo la kuchukua nafasi ya mshambuliaji huyo mpya kutoka Azam Fc.
“Mbaraka amepata matatizo kule Afrika Kusini, hali ya hewa ya baridi imemletea matatizo ambayo kwa sasa yanamzuia kucheza hivyo wakati tunatazama hali yake tumemuita Bocco kwanza kuchukua nafasi,” alisema Madadi.
Taifa Stars itashuka dimbani kwa mara nyingine siku ya Jumatano dhidi ya Zambia katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya COSAFA inayoendelea kuchezwa huko Afrika Kusini baada ya kuichakaza bao 1-0 Bafana Bafana usiku wa kuamkia leo.