WASHINDI NA MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA TUZO ZA WATU ZILIZOFANYIKA JIJINI DAR

Mtangazaji maarufu Salim Kikeke wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC ametwaa taji la Mtangazaji wa Runinga Anayependwa katika toleo la kwanza la Tuzo za Watu za Tanzania au Tanzania People’s Choice Awards katika sherehe zilizofanyika Serena Hotel, Ijumaa jijini Dar Es Salaam.
Vipengele 11 (kumi na kimoja) vilikuwa vikishindaniwa. Mshindi katika kila kipengele ameibuka na zawadi ya shilingi milioni moja pamoja na tuzo. Chini ya orodha ni picha za tukio hilo.
ORODHA YA WASHINDI
1. MTANGAZAJI WA REDIO ANAYEPENDWA Millard Ayo – Clouds FM
2. KIPINDI CHA REDIO KINACHOPENDWA Amplifaya – Clouds FM
3.MTANGAZAJI WA RUNINGA ANAYEPENDWA Salim Kikeke – BBC Swahili
4. KIPINDI CHA RUNINGA KINACHOPENDWA Mkasi – EATV
5. MWANAMICHEZO ANAYEPENDWA Juma Kaseja – Yanga
6. MUONGOZAJI WA VIDEO ZA MUZIKI ZINAZOPENDWA Nisher
7. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIUME My Number One – Diamond
8. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIKE Yahaya – Lady Jaydee
09. MUIGIZAJI WA KIUME KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA King Majuto
10. MUIGIZAJI WA KIKE KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA Elizabeth ‘Lulu’ Michael
11. FILAMU INAYOPENDWA Ndoa Yangu
Salim Kikeke - BBC Swahili
Salim Kikeke wa BBC Dira ya Dunia, mshindi wa kipengele 
cha Mtangazaji wa Runinga Anayependwa, akizungumza
 machache baada ya kutangazwa.
4K0A3518
Mkongwe King Majuto akiwapa mashabiki wake heko kwa 
kumpigia kura. Ameshinda kipengele cha Muigizaji wa 
Kiume Anayependwa Kwenye Filamu. Pembeni ni Lulu 
Michael, mshindi wa Mwigizaji wa Kike Kwenye Filamu 
Anayependwa.
4K0A3607
Picha ya pamoja ya walionufaika katika Tuzo za Watu mjini 
Dar Es Salaam, Juni 27, 2014.
4K0A3436
Hamza Kasongo, mkongwe katika fani ya utangazaji 
Tanzania akimkabidhi Tuzo Salim Kikeke.
4K0A3253
Luca Neghesti na Nancy Sumari waandaaji wa shughuli ya 
Tuzo za Watu. Wao pia wanahusika na Bongo5.com.
4K0A3705
Salim Kikeke (katikati), Mtangazaji wa Runinga 
Anayependwa akiwa na Luca Neghesti na Nancy 
Sumari waandalizi wa Tuzo za Watu.
Jimmy Kabwe
MC Jimmy Kabwe akiwa kazini – Tuzo za Watu 2014.
Jacqueline Ntuyabaliwe
Jacqueline Ntuyabaliwe aka K-Lynn


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright 2025 EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo