Mbunge wa Arusha mjini, Mh. Godbless Jonathan Lema amedai Vyombo vya usalama vimezuia kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Moshi mjini Mh. Philemon Ndesamburo kwenye uwanja wa Mashujaa.
Hatua hiyo inakuja ikiwa tayari maandalizi yameanza kufanywa katika Uwanja wa Mashujaa kwa ajili ya kuuga mwili wa Ndesamburo lakini OCD Moshi amezuia na kusema shughuli hiyo itafanyika Majengo badala ya Mashujaa kuepuka kuzuia shughuli za kila siku.