Mwenyekiti wa ACT Wazalendo ateulliwa na Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 03 Juni, 2017 amemteua Bibi Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Bibi Anna Elisha Mghwira anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Saidi Meck Sadiki aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Meja Jenerali Issah Suleiman Nassor kuwa Balozi.

Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Issah Suleiman Nassor alikuwa Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Halikadhalika, Mhe. Rais Magufuli amemteua DIGP Abdulrahman Omari Juma Kaniki kuwa Balozi.

Kabla ya uteuzi huo DIGP Abdulrahman Omari Juma Kaniki alikuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi.

Tarehe ya kuapishwa kwa wateule wote itatangazwa baadaye.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
03 Juni, 2017


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo