Godbless Lema ashangazwa na zuio la kuagwa kwa Ndesamburo

Mbunge wa Arusha mjini, Mh. Godbless Jonathan Lema amedai Vyombo vya usalama vimezuia kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Moshi mjini Mh. Philemon Ndesamburo kwenye uwanja wa Mashujaa.

Kupitia ukurasa wake wa twitter Mh. Lema amedai kuwa amezungumza na Diwani wa kata ya Sombetini Mh. Ally Bananga na kwamba wamezuiliwa na vyombo vya usalama kufanyia hapo shughuli ya kumuaga Mzee Ndesamburo.

"Nimeongea na Mh Bananga aliyeko uwanja wa mashujaa , vyombo vya usalama vinazuia kuaga mwili wa Ndesamburo kuagwa hapo. Hii ni mbaya sana" - Mh. Godbless Lema.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo