Wakati taifa likitilia mkazo utunzaji wa mazingira
kufuatia kuharibika kwa mazingira katika maeneo mbalimbali hapa nchini,
Wananchi wilayani Makete mkoani Njombe wameagizwa kuzingatia utunzaji wa
Mazingira
Hayo yamebainika hii leo wakati wa maadhimisho ya siku ya
mazingira duniani ambayo kiwilaya yamefanyika katika kata ya Mang'oto wilayani
Makete
Katika Maadhimisho hayo mgeni rasmi pamoja na wageni
mbalimbali alioongozana nao walishiriki zoezi la kukata miti ya kigeni
iliyopandwa kwenye chanzo kimoja cha maji katika kijiji cha Mang'oto, kama
ishara ya kutunza vyanzo vya maji visiharibiwe na miti isiyo rafiki na
mazingira
Akihutubia wananchi waliofika katika maadhimisho hayo kwa
niaba ya Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Makete, Afisa Mipango Eliab Simba
amesisitiza umuhimu wa kutunza mazingira, kwa kuwa athari za uharibifu wa
mazingira zimeshajitokeza katika maeneo mbalimbali hapa nchini
Awali akisoma Risala kwa mgeni rasmi, Mratibu Elimu kata
ya Mang'oto Bw. Mengi Chalamila amezungumzia uharibifu wa mazingira katika kata
yake na hatua zilizochukuliwa huku akipendekeza halmashauri kuongeza kiwango
cha faini kinachotozwa kwa kuwa vitendo vya uharibifu wa mazingira vimekuwa
vikitokea mara kwa mara
Kwa upande wake diwani wa kata ya Mang'oto Mh. Osmund
Idawa ametoa rai kwa wananchi kuendelea kutunza mazingira na kuepuka uchomaji
moto ovyo hasa wakati huu wa kuelekea kiangazi ili kuongeza manufaa
yanayotokana na utunzaji wa mazingira
Maadhimisho hayo kwa mwaka huu yanaongozwa na kaulimbiu
isemayo hifadhi mazingira muhimili kwa Tanzania ya viwanda
Zoezi la kufyeka miti isiyo rafiki katika chanzo cha Maji kijiji cha Mang'oto
Mti huo Baada ya Kukatwa hii leo
Miti iliyorafiki na chanzo cha Maji ikiwa imepandwa katika chanzo hicho cha maji
Mgeni rasmi akipokea Risala kutoka kwa Afisa Mtendaji wa kata ya Mang'oto Bw. Mengi Chalamila