Usiku wa June 3 2017 katika uwanja wa Millenium jiji la Cardiff nchini Wales Real Madrid waliandika historia mpya katika uwanja huo baada ya kufanikiwa kutwaa taji lao la 12 la UEFA Champions League katika historia ya club yao.
Real Madrid walitwaa taji hilo baada ya kufanikiwa kuifunga Juventus ya Italia kwa jumla ya magoli 4-1, baada ya ushindi huo wa Real Madrid leo June 4 wamewasili nyumbani kwao Hispania na kupata mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki wao.
Baada ya kuwasili Hispania Real Madrid walikaribishwa katika ukumbi wa City Hall jijini Madrid na baadae kutoka nje kuwasalimia maelfu ya mashabiki wao waliyojitokeza kufurahia ushindi huo, sherehe za Ubingwa wa Madrid zinaendelea usiku wa leo katika uwanja wao wa Santiago Bernabeu.