Mgeni rasmi (kwa niaba ya Mkuu wa wilaya) Eliab Simba akimpa mtoto chanjo katika uzinduzi wa chanjo Kiwilaya(Picha/Habari na Edwin Moshi)
-----------
Imeelezwa kuwa suala la kumpeleka mtoto kliniki kupatiwa
chanjo sio la Mama peke yake badala yake baba naye anawajibu wa kufanya hivyo
kwa mtoto wake
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Makete Mh
Veronica Kessy katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Afisa Mipango wilaya
ya Makete Eliab Simba katika zoezi la ufunguzi wa wiki ya chanjo iliyofanyika
kiwilaya Katika kijiji cha Ndulamo wilayani hapa
Amesema kumekuwa na dhana potofu iliyojengeka kwa jamii
kuwamba jukumu la kuwapeleka watoto kupatiwa chanjo ya kuwakinga na magonjwa
mbalimbali kuwa ni la mama peke yao jambo ambalo si la kweli na badala yake
wazazi wote wawili washirikiane pamoja kuwapeleka watoto wao kupatiwa chanjo
Akitoa taarifa ya mwenendo wa chanjo Kiwilaya kwa kipindi
cha januari hadi Machi mwaka huu, Kaimu Mganga mkuu wilaya ya Makete Bw.
Boniphace Sanga amesema watoto waliotarajia kupata chanjo ya kifua kikuu
walikuwa 1014 lakini waliochanjwa ni 881 sawa na asilimia 87
Baadhi ya wazazi waliowaleta watoto wao kupatiwa chanjo
wameelezea furaha waliyonayo huku wakiwahimiza wale wenye tabia ya kutowapeleka
watoto kupatiwa chanjo kuacha mara moja
Wiki ya chanjo kiwilaya imezinduliwa leo Aprili 24 na
itaendelea hadi Aprili 30
Kaimu Mganga Mkuu wilaya ya Makete Boniphace Sanga akitoa taarifa kwa Mgeni Rasmi
Mwakilishi wa Mgeni Rasmi akitoa hotuba yake
Hotuba ikiendelea
Wananchi wakisikiliza hotuba ya mgeni Rasmi
Kina mama wakifurahi baada ya watoto wao kuchanjwa na mgeni Rasmi
Ukaguzi wa kadi za watoto uiendelea kabla ya kupatiwa chanjo