Akizungumza na blog hii Afisa Afya wa kata ya Tandala
Bw. Huruma Mkiramweni amesema kuwa wamefanya ukaguzi huo katika kijiji cha
Tandala kwa wafanya biashara na kubaini bidhaa zenye thamani ya zaidi ya
shilingi laki sita zimekamatwa zikiwa zimeisha muda wake wa matumizi.
Mkiramweni anelezea sheria ambazo zitachukuliwa kwa
mfanya biashara pindi anapokutwa na bidhaa zilizokwisha muda wake wa matumizi
kuwa faini yake ni kuanzia shilingi laki moja hadi milioni moja
Afisa mtendaji wa kata ya Tandala Bi, Kalemela Marley
amesema kuwa kutokana na ukaguzi walioufanya kwa kijiji cha Tandala wamebaini
kuwa kuna baadhi ya watu wanauza vitu
vilivyokwisha muda wake wa matumizi tangu mwaka 2014 na mchakato huo utafanyika
kwa kata nzima.