Wito umetolewa kwa wananchi walioko kwenye hifadhi ya barabara ya Njombe
Makete kutii agizo la serikali la kubomoa nyumba zao kwa hiari ambapo Machi 26 mwaka huu ndiyo
siku ya mwisho Ya kutekeleza agizo hilo kwa hiari.
wakizungumza na blog hii baadhi ya wahusika wa bomoa bomoa hiyo
wamewasihi ambao hawajabomoa kutii agizo la serikali kwakuwa barabara ya lami
waliomba wenyewe kujengewa na itakuwa na maendeleo kwao.
Aidha wananchi hao wamesema kuwa matarajio yao makubwa ni serikali kujenga
barabara hiyo ya lami kwa wakati japo wengine wamelipokea vizuri wengine vibaya
japo maendeleo yana hitaji kugaramiwa.









