Wazawa wapenda maendeleo kutoka nje ya kijiji cha Ndulamo
Kata ya Iwawa wilayani Makete mkoani Njombe wameendelea kuunga mkono serikali
na jitihada za wananchi wa kijiji hicho za ujenzi wa shule mpya ya msingi
Kiduga iliyopo kijijini hapo
Kufuatia hali ya ujenzi wa vyumba vingine vitatu vya
madarasa pamoja na ofisi za walimu inayoendelea shuleni hapo, wazawa hao
wamechangia bati 76, misumari kilo 25, vyote vikiwa na thamani ya shilingi
milioni moja laki saba na elfu themanini na moja (1,700,081)
Akitoa taarifa hiyo afisa mtendaji wa kijiji cha Ndulamo
Majuto Mbwilo amesema pamoja na kuwa utawasogeza kwa kiasi kikubwa na
kuwapunguzia gharama, lakini bado wanauhitaji wa michango ya wadau mbalimbali
ili kazi hiyo iweze kumalizika kwa wakati
Amesema shule hiyo imeanza kutumika tayari kuanzia mwezi
huu ambapo kwa kuanzia wamepewa walimu watatu, na madarasa matatu kwa maana ya
darasa la awali, la kwanza na la pili ikiwa na jumla ya wanafunzi 118
Mtendaji huyo akatumia fursa hii kutoa onyo kwa wazazi au
walezi ambao hawatapeleka watoto wao shule licha ya jitihada hizo zinazofanywa
kuwa sheria haitawaacha
Sikiliza Sauti Hapa Chini:-