Inasikitisha; Moto walipuka Hospitali ya Rufaa mkoa wa Kagera

Wodi ya saba ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera imenusurika kuteketea baada ya kuzuka kwa moto ambao umesababisha kifo cha mtu mmoja ambaye ametajwa kwa jina la Jackson Didas mkazi wa kata ya Hamgembe iliyoko katika manispaa ya Bukoba ambaye ni mtoto anayekadiliwa kuwa na umri wa mwaka mmoja na nusu aliyekuwa amelazwa katika wodi hiyo huku akiwa mahututi. 

Kwa mujibu wa Emmanuel Mathewa muuguzi wa zamu aliyeshuhudia tukio hilo ameeleza kwamba moto huo ulizuka jana majira ya saa 10 jioni na amedai umesababishwa na wazazi wa mtoto huyo aliyefariki ambao walitoroka na mwili wa marehemu huyo baada ya tukio hilo, amesema wazazi hao walikuwa wamewasha moto ndani ya wodi hiyo waliokuwa wakiutumia kumfukiza marehemu huyo kwa dawa za kienyeji wakati huo akiwa amewekewa mashine ya kupumulia. 

Kwa upande wake, katibu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera Kilwanila Kiiza amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na ameeleza kuwa marehemu huyo alilazwa katika hospitali hiyo Januari 16, mwaka huu na alikuwa na homa kali iliyokuwa imeambatana na hali ya utapiamulo, amesema alikuwa akipata matibabu katika hospitali hiyo hadi alipopatwa na mauti yalisababishwa na wazazi wake ambao anadai hadi sasa hawajulikani walipo. 
  
Hadi tunatuma taarifa hii kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Augustine Ullomi alikuwa nje ya ofisi kikazi, hata hivyo mmoja afisa wa ngazi ya juu katika jeshi hilo ambaye ameombwa jina lake lisitajwe kwa kuwa sio msemaji amekiri kuwa jeshi hilo limepokea taarifa za kifo cha marehemu huyo na linazifanyia kazi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo