Akitoa taarifa ya hali ya barabara hiyo, Diwani wa kata
ya Ukwama Mh. Agustino Tweve amesema hali ya barabara hiyo katika baadhi ya
maeneo sio nzuri na endepo mvua zitaendelea kunyesha mawasiliano ya barabara
hiyo yatakatika na kusababisha magari hasa basi la abiria linalokwenda Ukwama
kukatisha safari zake
Amesema mpango wa kuikarabati barabara hiyo upo na tayari
fedha zimeshatengwa lakini kinachokwamisha hivi sasa ni mvua zinazoendelea
kunyesha, lakini pamoja na hayo wamemuomba mkandarasi atakayejenga barabara
hiyo kufanya marekebisho katika maeneo korofi ili barabara hiyo iendelee
kupitika
Hata hivyo diwani huyo ametaja sababu za kuharibika kwa
barabara kuwa ni pamoja na kuziba mifereji ya kupitishia maji hali iliyopelekea
maji kupita barabarani, pamoja na magari yenye uzito mkubwa kuliko uwezo wa
barabara kupita katika barabara hiyo
Mkurugenzi wa kampuni ya Asajile Builders Limited
itakayofanya matengenezo ya barabara hiyo Bw. Asajile Mbwilo amewahakikishia
watumiaji wa barabara na wananchi kwa ujumla kuwa itapitika baada ya
marekebisho atakayoyafanya hivi karibuni
Mkandarasi huyo ameomba ushirikiano wa kutosha kwa
wananchi kwani serikali peke yake haiwezi kufanya hayo, lakini ushirikiano wa
pamoja ndio utawezesha matengenezo ya barabara hiyo kukamilika huku akiwasihi
wananchi kuwa mstari wa mbele kutunza miundombinu hasa barabara ili ziweze
kudumu kwa muda mrefu