Majangili 7 wakamatwa Hifadhini Morogoro

Kufuatia kukithiri kwa vitendo vya ujangili katika hifadhi ya wanyama pori ya wamimbiki iiliyopo katika wilaya za Morogoro, Mvomero pamoja na Bagamoyo askari wa hifadhi hiyo wamefanya operesheni na kufanikiwa kukamata majangili saba pamoja na roli lililosheheni mbao na magogo huku makundi ya mifugo na matanuru ya mkaa yakionekana kuwa moja ya sababu ya uharibifu wa hifadhi hiyo.

Akizungumza mara baada ya operesheni hiyo mwenyekiti wa jumuiya ya hifadhi ya Wamimbiki Bwana Omary Tofiki amesema hifadhi hiyo ipo hatarini kutoweka kufuatia kuvamiwa na makundi ya mifugo, uchomaji mkaa kupita kiasi, uchanaji mbao pamoja na uwindaji haramu wa wanyama pori.

Aidha mwenyekiti huyo amesema ili kuinusuru hifadhi hiyo amemuomba rais Dokta John Pombe Magufuli kuwasaidia magari kwa ajili ya doria za mara kwa mara pamoja na fedha za uendeshaji kwa sasa hifadhi hiyo haiwezi kujiendesha yenywe kutokana na ufisadi uliofanywa na viongozi wa jumuiya ya hifadhi hiyo waliomaliza muda wao.

Kwa upande wao watuhumiwa wa ujangili katika hifadhi hiyo wamesema wao ni vibarua wa matajiri wanaowatuma kuwafanyia kazi na kwamba wapotayari kuwataja matajiri hao.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo