Majambazi wavamia duka la mfanyabiashara mkoani Kigoma

Watu watatu wamejeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kigoma baada ya watu sita wanaosadikiwa kuwa majambazi wakiwa na bunduki mbili na mapanga kuvamia duka la mfanyabiashara mmoja mjini Kigoma na kupora fedha na mali nyingine. 

Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Ferdinand Mtui amesema watu hao wakiwa wameficha silaha katika makoti waliyokuwa wamevaa waliingia dukani kama wateja na baada ya kupora waliwajeruhi watu hao kwa risasi na kukimbia na kwamba watu wawili wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Mmoja wa majeruhi katika tukio hilo Hussein Issa ambaye aliporwa zaidi ya shilingi laki mbili pamoja na simu alizokuwa akizitumia kutuma na kupokea pesa kutoka kwenye mitandao mbalimbali amesema tukio hilo lililotokea majira ya saa mbili usiku ambapo watu hao waliingia kama wateja na baada ya kukaidi amri waliyoitoa ndipo walipotumia bunduki ambapo mganga mfawidhi katika hospitali ya mkoa wa Kigoma Maweni Dk Fadhil Kibaya amesema juhudi zinafanya kutoa risasi ambazo zipo mwilini.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo