Bangi ya kufa mtu yakamatwa Huko Kigoma

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limemkamata mkazi mmoja wa kijiji cha Matyazo tarafa ya Kalinzi wilayani Kigoma akiwa na zaidi ya miche 150 ya Bangi katika shamba lake, miche ambayo imeng’olewa na wananchi na kuiteketeza huku wananchi wakilalamikia kuongezeka kwa uhalifu katika eneo. 

Mkazi huyo wa kijiji cha Matyazo Madua Saidi amekamatwa baada ya kuwepo kwa taarifa juu yake kuhusika na biashara ya bangi, ambapo mara baada ya kukamatwa mwenyekiti wa kijiji cha Matyazo Patrich Kezron pamoja na wananchi wameitaka serikali kuendesha msako vijijini kutokana na kushamiri kwa kilimo cha bangi ambacho kimekuwa kikiharibu afya za wananchi na kuzorotesha uchumi maelewano katika familia na jamii.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma kamishna msadizi mwandamizi wa polisi Ferdinand Mtui amesema mtuhumiwa huyo ambaye atafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika amelima bangi hiyo pamoja na mazao mengine ili isitambulike kirahisi na kwamba msako mkali unaendelea mashambani ili kuwasaka wakulima wanaolima bangi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo