Bomoa Bomoa Yaacha Vilio Meatu, RPC aonya wanaovaa Tisheti za Njaa Inauma

Wananchi wa vijiji vya Mwabagimu na Bukundi wilaya ya Meatu wamelalamikia kitendo cha kubomoa nyumba 15 za familia 4 kulikofanywa na kampuni moja ya udalali katika kutekeleza amri ya Mahakama iliyompa ushindi Joseph Masibuka dhidi ya Ngusa Machimu kufuatia mgogoro wa Ardhi uliohuisisha hekari 70 uliodumu muda mrefu.
Wakizungumza na Waandishi wa Habari baadhi ya wananchi walioshuhudia zoezi hilo likiteketeza magodoro, nyumba kubomolewa na zingine kuchomwa moto wamekilaani kitendo hicho walichokiitwa ni cha kikatili na kuomba waliohusika kuchukuliwa hatua sitahiki ,huku mwanamke mmoja mwenye mtoto mchanga akilia kwa uchungu kwa kubomolewa nyumba na kuishi nje akipigwa baridi kali.
Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya meatu na kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa simiyu iliyoongozwa na mkuu wa wilaya ya meatu dkt joseph chilongani iliyotembelea maeneo yote nyumba zilizobomolewa na baadhi kuchomwa moto na kukutana na baadhi ya wahanga na wengine wameyakimbia makazi yao kwa hofu ya kukamatwa wakabaini nyumba zote zilizobomolewa ziko nje ya eneo la ekari 70 lenye mgogoro lililompa ushindi joseph masibuka ambaye ni diwani wa kata ya Bukundi ,baada ya kamati hiyo kupitia mipaka ya shamba hilo kwa kuwatumia watalaam wa ardhi kwa kupima eneo hilo na kujiridhisha ukubwa wake na hivyo kutolewa maamuzi ya serikali katika mkutano wa hadhara.
Kaimu kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu Kamishina Msaidizi Jonathan Shanna amewapongeza wananchi kwa kutojichukulia sheria mkononi wakati zoezi hilo linatekelezwa na kuwasihi kutofanya visasi vyovyote na pia akatumia hadhara hiyo kuwaonya waliochapisha tshirt zenye maadishi ya njaa inauma hazina nafasi simiyu.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo