NAIBU waziri wa nishati na madini Medard Kalemani amemuagiza Kamishina wa madini nchini Tanzania Ally Samage kurusha aliyekuwa Afisa Madini Mkoa wa Geita Fabiani Mshai hili kujibu baadhi ya hoja za kamati ilioundwa juu ya ukaguzi uliokuwa ukifanyika ndani ya Mgodi RZ uliofunika watu 15.
Ametoa kauli hiyo kwenye kikao cha kamati ya ulinzi na usalama wa Mkoa huo baada ya kumaliza kuokoa watu 15 walikuwa wamefukiwa na kifusi ndani ya Mgodi huo uliko kijiji cha Nyarugusu Wilaya na Mkoa wa Geita.
Kalemani amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kulikuwa na uzembe mkubwa kwa wakaguzi ndani ya Mgodi huo hivyo kuchukua uamzi wa kumrudisha Afisa Madini huyo aliyeamia Mkoa wa Simiyu hili kujibu baadhi ya Tuhuma.
Kalemani ameongeza kutokana na kutokea kwa hali hiyo ndani ya Mgodi huo unaomilikiwa na Amedi Mbaraka pamoja na Raiya wa china Serikali imejipanga kuchukua tahadhali kwenye Migodi ya wachimbaji wadogo wadogo nchini.
Kwa upande wa makampuni yaliojitolea mashine na vifaa mbalimbali waliokuwa wanafanya uokoaji ndani ya Mgodi huo walikuwa na haya ya kusema mbele ya Channel Ten.
Watu hao 15 walizama ndani ya Mgodi wa RZ ulikoko katika kijiji cha Mawe Meru kata ya Nyarugusu Wilaya na Mkoa wa Geita unaomilikiwa na Amedi Mbaraka wameokolewa jana wote wakiwa wazima na kupewa uduma ya kwanza kisha kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita kwa matibabu zaidi.