WATU 15 waliokolewa ndani ya Mgodi wa RZ ulioko katika kata ya Nyarugusu Wilaya na Mkoa wa Geita na kupelekwa katika Hospitali ya Mkoa kwa matibu zaidi wameruusiwa na kwenda Nyumbani kwao baada ya hali zao kuimalika.
Blog hii imefika katika Hospiatali ya Mkoa wa Geita majira ya asubuhi na kukuta watu hao wakiwa wamebadilika taofauti na walivyokuwa siku ya jana wakati wanaokolewa kwenye shimo hilo walilokaa kwa siku nne.
Wakizunguma mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Msitaafu Ezekieli Kyunga aliyefika kwa lengo la kuwajulia hali wamesema wanawashukuru watanzania kwa kuwaokoa na kuiomba Serikali kushirikina na Mgodi huo kuongeza ujira wakati wa kazi kwani wanafanya kazi ngumu.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali Mkuu wa Mkoa wa Geita EZEKIELI KYUNGA amesema hiyo ni ajali kama ajali nyingine .
Watu hao waliokolewa jana majira ya saa tano na nusu asubuhi na kupelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Geita ambapo leo wote wakiwa na afya njema wameachiwa kwenda Nyumbani.
