Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoa wa Mwanza ametangaza kuwafuta kazi maafisa tarafa, watendaji wa kata na mitaa watakao legalega kuwadhibiti wafanya biashara ndogondogo machinga baada ya oparesheni inayoendelea.
Akizungumza na Waandishi wa habari Mkuu wa wilaya hiyo Mery Tesha amesema kuwa baada ya zoezi la kuwaondoa machinga katikati ya jiji la Mwanza wametoa mamlaka kwa maafisa hao kuhakikisha hakuna watu watakao tenga biashara zao maeneo yasiyo rasmi.
Bi. Tesha ameeleza kuwa mpaka sasa kuna wafanya baishara walioondolewa katikati ya jiji lakini wameanza kurudi kinyume na amri ya wao kuondoka na kuanza kuwashambulia migambo hivyo maafisa waliopewa dhamana wakishindwa kuwadhibiti watafukuzwa kazi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Machinga mkoa wa Mwanza Saidi Tembo ame amesema kuwa licha ya serikali kuwaondoa machinga mjini wengine wamekosa maeneo ya kufanyia biashara kulingana na idadi yao.