Makete.
Mwanaume aliyefahamika
kwa jina la Bahati Marukusi Nyaluke ambaye umri wake unakadiriwa kuwa miaka
zaidi ya (40 )amekutwa amejinyonga chumbani kwake jioni ya Desemba 8 mwaka huu
eneo la Kilovoko kijiji cha Tandala wilayani Makete mkoani Njombe.
Taarifa kutoka
eneo la Tukio zinadai kuwa mwili huo ulionwa na mwanaye ambaye ni Husseni
Bahati (21) kisha kutoa taarifa kwa watu wengine.
Polisi kutoka
kituo cha polisi Tandala wamefika eneo la Tukio na kufanya ukaguzi wa mwili wa
marehemu kisha kutoa ruhusa ya kuushusha mwili huo kutoka kwenye kamba ili kuendelea na taratibu zingine za jeshi
hilo.
Mpaka mwandishi wa
eddy blog anaondoka kwenye eneo la Tukio usiku huu Disemba 8 taarifa za kuuzika
mwili wa marehemu zilikuwa hazijathibitishwa na jeshi la polisi na kwamba
zitatolewa na mamalaka husika ya jeshi la polisi usiku huu ama asubuhi ya Desemba
9 kama uzikwe ama uendelee kusubiri.
Chanzo cha kifo
cha marehemu bado hakijafahamika huku uchunguzi zaidi ukiendelea
Kwa taarifa za
awali Marehemu inadaiwa aliingia chumba cha pili ambacho hakina Dari kisha
kufunga kamba aina ya manila na akatoboa dari ya silin bodi akaitolea kamba
iliyotoka kwenye kenchi na akaingia chumbani mwake na kujifungia na kufanya
tukio la kutoa uhai wake.
Taarifa kamili za
tuio hilo zitakujia hapa baada ya kuzipata kutoka jeshi la polisi