Watumishi wanaosimamia hifadhi za taifa (TANAPA) pamoja na
maeneo mengine yaliyochukuliwa na serikali kwa ajili ya hifadhi wameagizwa
kuacha tabia ya kuwapa kipigo wananchi wanaozunguka maeneo yaliyohifadhiwa kwa
kuwa hali hiyo inaongeza migogoro badala ya kuitatua
Kauli hiyo imetolewa leo na mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt Rehema
Nchimbi katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika mkoani
hapo, ambapo amesema wananchi ndio majirani wakubwa wa maeneo hayo badala ya
kuwapiga wanatakiwa wawaelimishe pale wanapokosea badala ya kuwapiga kwa kuwa
hali hiyo inajenga chuki na migogoro kuongezeka
Mkuu huyo ameagiza mtumishi yeyote atakayempiga mwananchi
aliyekiuka sheria za hifadhi atachukuliwa hatua za kisheria hivyo kama
wakiwakamata wananchi waliokosea wanatakiwa kuwapeleka kwenye vyombo vya sheria
ili wachukuliwe hatua za kisheria badala ya wao kuchukua sheria mkononi kwa
kuwapiga
Uamuzi huo wa mkuu wa mkoa umetolewa baada ya kupokea taarifa
ya hali ya migogoro ya ardhi kwa wilaya zote za mkoa wa Njombe ambapo kwa
taarifa ya mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kessi imeeleza kuwepo kw
migogoro ya ardhi katika wilaya yake ikiwemo wananchi kuwa na migogoro na
hifadhi za taifa
Aidha Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe
Antony Mawata na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Egnatio Mtawa
wamezungumzia mgogoro baina ya wilaya hizo mbili unaosababishwa na ardhi na
wakaahidi kukaa pamoja kuumaliza mgogoro huo
Sikiliza sauti hapa chini:-