Mbuyu Twite Ndio Basi Tena Yanga

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara, Yanga wamethibitisha rasmi kuachana na mchezaji wao Mbuyu Twite na nafasi yake kuchukuliwa na Justine Zulu wa Zambia.
img_0398
Baraka Deud Edith amethibitisha kuachwa kwa Twite wakati alipokuwa akiongea na Radio EFM katika kipindi cha Sports HQ.
Aidha sheria za TFF kwa timu za ligi kuu zinasema kuwa kila timu ya ligi kuu inapaswa kusajili wachezaji wasiozidi saba, hivyo Yanga walikuwa na wachezaji nane.
Mkataba wa mchezaji huyo unamalizika mwezi huu wa Disemba huku akiwa na nafasi ya kufanya mazungumzo na timu yoyote inayo muhitaji kutokana na kanuni za sheria za mchezo wa soka.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo