Ishu ya Ukatili kwa wanafunzi, Polisi Wawekwa Mtu Kati

Baadhi ya wazazi wa wanafunzi wilayani pangani,wamelalamikia jeshi la polisi kwa kushindwa kuchukua hatua kali za kisheria kwa baadhi ya watuhumiwa wanaowafanyia wananfunzi vitendo vya kikatili ikiwemo ubakaji hatua ambayo imesababisha wanafunzi kushindwa kufikia ndoto zao.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Tungamaa kilichopo kata ya mwera wilayani Pangani,mmoja kati ya wazazi hao amesema matukio kadhaa yameripotiwa ya ubakaji na wanapofikisha katika vyombo vya sheria baadhi ya watuhumiwa wanatoroshwa hatua ambayo inachangia ongezeko la vitendo hivyo.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa na kamati za kukabiliana na maambukizi ya ukimwi,afisa ufuatiliaji na mafunzo wa shirika la kutetea haki za watoto wilayani pangani kenned mashema amesema jitihada zinazofanywa na wanaharakati kwa kushirikiana na serikali kwa kiutoa elimu kuhusu madhara ya ukatili kwa wanafunzi,wazazi wamefanikiwa kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa kusaidiwa na serikali lakini ukosefu wa mabweni umeendelea kuathiri wananfunzi.

Kufuatia hatua hiyo,mkuu wa wilaya ya pangani zainab issa amekemea vikali tatizo la ucheleweshai wa kesi za ukatili dhidi ya wanafunzi na amewaagiza viongozi wa serikali ngazi za vijiji hadi kata kuwafichua watuhumiwa ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo