Watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha za moto wamevamia kwenye machimbo ya dhahabu ya Nholi yaliyopo wilayani Bahi mkoani Dodoma na kuwaua wachimbaji wadogo wawili na kujeruhi wengine wanne na kupora madini na fedha ambazo thamani haijafahamika na kisha kutokomea kusikojulina.
Wakizungumza kwenye wodi namba moja iliyopo hosipitali ya rufaa ya Dodoma baadhi ya majeruhi wa tukio hilo wanaeleza namna majambazi hayo yalivyovamia na kisha kufanya unyama huo kabla ya kutokomea.
Mganga mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. James Charles amethibitisha hosipitali hapo kupokea miili ya marehemu wawili waiouawa na majambazi hao
Jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Lazaro Mambosasa ili kuzungumzia tukio hilo zimeshindikana baada ya kutafutwa mara kadhaa na kisha ikafahamika kuwa yupo nje ya mkoa kikazi.