Baada ya mkulima kuchomwa Mkuki Morogoro baadhi ya wafugaji wayakimbia makazi yao

Tukio la wafugaji kuwashambulia wakulima katika kijiji cha Dodoma Isanga wilayani kilosa mkoani Morogoro kulikosababisha Augustino Pius kuchomwa mkuki limechukua sura nyingine baada ya baadhi ya wafugaji kuyakimbia makazi yao kwa madai ya kuhofia usalama huku wakiiomba serikali kuchukua hatua kuinusuru mifugo iliyokatwa mapanga siku ya tukio.
Pitapita ya Mwandishi wa habari hii imeshuhudia wafugaji wengi wakiwa wameyahama makazi yao na kuelekea porini wakidai kuhofia usalama wao mara baada ya watu 12 kukamatwa kwa makosa ya kuwashambulia na kuwajeruhi wakulima aidha wamesema kutokana na tukio hilo ng`ombe 17 walijeruhiwa hali ambayo inawapelekea kuiomba serikali kuhakikisha wanatenga maeneo ya wakulima na wafugaji ili kuondoa migogoro iliyopo.
Kwa upande wake naibu katibu wa chama cha wafugaji Tanzania Joshua Lugaso ameiomba serikali kuagiza maafisa mifugo kutoa msaada wa awali kuinusuru mifugo iliyojeruhiwa na mapanga huku mkuu wa wilaya ya kilosa adamu mgoyi amesema kuwa maeneo yote yaliyotengwa kwa mujibu wa mapitio ya baraza la madiwani ya mwaka 2001 lililopitisha kuwa vijiji saba ni kwa ajili ya wafugaji na vilivyobakiani kwa ajiri ya kilimo .


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo