Mtuhumiwa aliyemchoma Mkuki Mkulima Morogoro akamatwa

Mtuhumiwa aliyemchoma mtu mkuki wa Mdomoni Ukatokea shingoni mkoani Morogoro ametiwa Mbaroni

Tukio hilo, llilitokea Desemba 25, mwaka huu katika shamba la Dotto Mfaume, baada ya wafugaji kuingiza mifugo yao na Mtitu kuamua kuwafukuza baada ya mkulima mwenzake kuomba msaada.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Urlich Matei, alisema mtuhumiwa alikamatwa Desemba 28, kufuatia msako uliofanywa na jeshi hilo kata ya Masanze.

Alimtaja mtuhumiwa kuwa ni Amani Joseph, maarufu kama Matonya, mgogo ambaye alikuwa ni mchunga ng’ombe na mkazi wa kijiji cha Miyombo, wilayani Kilosa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo