ZAIDI ya kaya 3000 katika kijiji cha Itunduma kata ya Mtwango katika Halmashauri ya wilaya ya Njombe mkoani Njombe zimeondokana na tatizo la uhaba wa maji baada yakukamilika kwa mradi wa maji uliojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 65.
Moja ya changamoto kubwa zinazowakabili wananchi wa kijiji cha Itunduma ni upatikanaji wa maji ambao wakati wote uliwalazimu kutembea umbali mrefu kutafuta maji.
Mkazi mmoja kijijini hapo Bw Antony Mwandulami ambaye anajishughulisha na utoaji wa tiba za asili anajitokeza na kumaliza tatizo hilo kwa kujenga mradi wa maji kuwataka watanzania kwote nchini kuona namna ya kumaliza matatizo ktk maeneo yao badala ya kusubiri serikali kufanya hivyo wakati wote.
Naye Mwenyekiti wa kijiji hicho, Bw Medson Nyagawa amesema mradi huo umekuwa wa mafanikio makubwa kijijini hapo.