Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amesema rushwa ni kansa ya maendeleo kwa nchi ya Tanzania hivyo inatakiwa kupigwa vita.
Akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari nchini Ikulu jijini Dar es salaam, Rais Magufuli amesema kuwa rushwa imekuwa ikilitesa taifa.
“Nyinyi wenyewe waandishi wa habari mnaona jinsi rushwa ilivyokuwa imetawala katika nchi yetu, lakini kwasasa watu wamekuwa na adabu na kazi, watu wamekuwa wakiheshimu kazi, tumekuwa tukipiga vita rushwa na nyinyi mnaona kwasababu rushwa ni kansa ya maendeleo katika taifa letu tuikwepe,” amesema Magufuli.
Ijumaa hii rais Magufuli yupo katika mahojiano maalumu na waandishi wa habari Ikulu Dar es salaam.