Rais Dkt John Magufuli amesema suala La katiba Mpya sio kipaumbele cha serikali yake na hakuna sehemu yeyote alipooahidi wakati wa kampeni kuwa atashughulikia ratiba mpya
Rais Magufuli ameyasema hayo Ikulu jijini Dar Es Salaam wakati Akizungumza na vyombo vya habari Ikulu jijini DSM muda huu
Rais amesema mchakato wa katiba Mpya usubiri kwanza na kwa sasa ameamua kuinyoosha nchi ili ikae kwenye mstari mzuri
"Kwa sasa naomba mniache ninyooshe nchi" amesema Rais Magufuli